Image post
Instagram

Bado kuna haja ya kuongelea hili. Kuna siku nilienda kumtembelea bi mkubwa wangu kwake.Wakati nafika yeye hakuwepo.Hivyo ilibidi nimsubiri maana alisema asinge kawia. Basi alivyofika tu baada ya salamu akaanza "Yaani nimetoka kuamua kesi huko, kuna mwanafunzi wa darasa la sita ana ujauzito." Nikashtuka sana. Mama yangu ni mwanakamati wa shule ya msingi jirani na nyumbani. Akaendelea "Cha kuhuzunisha zaidi aliyempa mimba ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari jirani" Nikashtuka zaidi. Yaani ni shida tupu.Mtoto amempa mimba mtoto."Very tricky" Masomo haya yanaanzwa kufundishwa mapema sana.Hii yote ni kwa sababu watoto wanatakiwa watambue mapema sana madhara ya vitu hivi.Lakini swali la kujiuliza ni ... Kwa nini bado kesi hizi zipo sana? Walimu mashuleni tuendelee kutia mkazo haswaa tukifika kwenye mada hizo.Lakini wazazi ni wakati sasa umefika ongea na mwanao ingali mapema sana.Hakuna tena haja ya kuwaficha. Cha msingi tu tutafute maneno na njia sahihi ya kuwafikishia ujumbe.SAFARI YA MALEZI NI NDEFU SANA NA KAMA INGELIKUWA NI SHULE BASI WOTE TUNGEKUWA MAPROFESA NDIO TUWE TUMEHITIMU. Stay safe. #earlypregnancy #pregnant #pregnancy #pupils #student #school #ujauzito #malezi #mfanyeaweborakulikojana #parenting @ummymwalimu @baba_keagan @mwijaku @diamondplatnumz @ommydimpoz @officialalikiba @harmonize_tz @hamisamobetto @officialshilole