Image post
Instagram

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tunu Juma Kondo amewataka wanafunzi wa Skuli ya Chumbuni kujikinga na vitendo vya udhalilishaji na mimba za utotoni. Akitoa elimu ya kujikinga na vitendo hivyo katika Skuli ya Chumbuni Msingi, Tunu amewataka wanafunzi kujiepusha kupokea zawadi ama pesa kwa watu wasiowafahamu. Amewashauri wanafunzi wa skuli hiyo kutokubali kupakiwa kwenye gari za watu ambao hawawajui kwani ni miongoni mwa mbinu zinazotumiwa na vijana wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kukamilisha malengo yao #ccm #uwt #ubakaji #rapedits #woman #womans #womansright #womansrights #chumbuni #zanzibar #pregnants #earlypregnancy #avoid #wisewords #wise #stop #zanzibar24habari